Masharti kwa SoteApp
Kukubaliana na Masharti
Kwa kupakua, kutizama, au kutumia SoteApp (inayojulikana kama “App”), unakubali kufuata na kuwa chini ya Masharti haya. Ikiwa hukubaliani na Masharti haya, hutaruhusiwa kutumia App hii.
Ustahiki
• Lazima uwe na umri wa angalau miaka 18 ili kutumia App.
• Kwa kutumia App, unawakilisha na kuthibitisha kwamba una uwezo wa kisheria kuingia katika Masharti haya.
Akaunti ya Mtumiaji
• Inawezekana ukahitaji kutengeneza akaunti ili kupata huduma za App.
• Unawajibika kudumisha siri kwa taarifa za akaunti yako na kwa shughuli zote zinazofanyika chini ya akaunti yako.
• Unakubali kutoa taarifa sahihi na za kisasa wakati wa usajili.
Shughuli Zilizozuiliwa
Unakubali kutofanya yafuatayo wakati wa kutumia App:
• Kuweka orodha za bidhaa au huduma zinazodanganya, kupotosha, au udanganyifu.
• Kutumia App kwa madhumuni yoyote si ya kisheria au yasiyoruhusiwa.
• Kuharasi, kutishia, au kudhuru watumiaji wengine.
• Kuvunja sheria au kanuni yoyote ya nchi
• Ku upload ama kuweka maudhui yoyote yanayokera, ya kudhalilisha, au yanayovunja haki za miliki ya akili.
• Kutumia zana za moja kwa moja (kama vile bots, scrapers) kufikia au kuingiliana na App.
Matanganzo na Miamala
• Unawajibika kwa usahihi na uhalali wa tanganzo zako.
• App haiwajibiki kwa ubora, usalama, au uhalali wa bidhaa zilizotangazwa, wala ukweli wa bidhaa hizo.
• Miamala kati ya watumiaji (muuzaji na mnunuzi) ni kati ya pande zinazohusika pekee. App sio sehemu ya muamala wowote na inajiondoa na dhima yoyote inayotokana na miamala hiyo.
Ada na Malipo
• Baadhi ya huduma za App zinaweza kuhitaji malipo ya ada.
• Unakubali kulipa ada zote na kodi zinazohusiana na matumizi yako ya App.
• Ada hazirudishwi isipokuwa ilivyoainishwa vinginevyo.
Haki za Miliki wa App
• App na maudhui yake (kama vile nembo, maandiko, michoro) ni mali ya SoteApp na inalindwa na sheria ya umiliki ya Zanzibar.
• Huwezi kunakili, kubadilisha, au kusambaza sehemu yoyote ya App bila idhini ya maandishi kutoka kwa SoteApp.
Faragha
Matumizi yako ya App yanategemea Sera yetu ya Faragha, ambayo inaelezea jinsi SoteApp tunavyokusanya, kutumia, na kulinda taarifa zako binafsi.
Kusitisha Matumizi
• SoteApp ina haki ya kusitisha au kukomesha utumiaji wako wa App wakati wowote, bila au kwa taarifa (kukujuilish), kwa sababu yoyote, ikiwa ni pamoja na kuvunja
Masharti haya
• Unaweza pia kufunga akaunti yako wakati wowote kwa kufuata maagizo yaliyopo kwenye App..
Kujiondoa na Kizuizi cha Dhima
• App inatolewa “kama ilivyo” na “kama inavyopatikana” bila dhamana yoyote, iwe wazi au iliyojificha.
• SoteApp haitawajibika kwa madhara yoyote ya moja kwa moja, au ya matokeo yanayotokana na matumizi yako ya App.
• Dhima yetu kwako ni kwa madai yoyote yanayotokana na au yanayohusiana na App haitazidi kiasi ulicholipa (ikiwa chochote) kwa kutumia App..
Sheria Inayotawala
Masharti haya yanatawaliwa na sheria za Zanzibar. Migogoro inayotokana na Masharti haya itatatuliwa katika mahakama ya Zanzibar.
Mabadiliko ya Masharti
•SoteApp tuna haki ya kubadilisha Masharti haya wakati wowote. Matumizi ya App baada ya mabadiliko yoyote yanajumuisha kukubali kwako Masharti yaliyorekebishwa.
Taarifa za Mawasiliano
Kwa maswali au wasiwasi kuhusu Masharti haya, tafadhali wasiliana nasi kupitia: soteapp1@gmail.com
Muhtasari
Masharti haya yanaelezea sheria na taratibu zinazotawala matumizi ya SoteApp. Yanajumuisha ustahiki wako kutumia app, majukumu yako katika kudumisha akaunti yako, vitendo vilivyokatazwa wakati wa kutumia App, na utunzaji wa miamala kati ya watumiaji. Aidha, yanaelezea kizuizi cha dhima, sera ya faragha, na jinsi mabadiliko kwenye masharti yatavyowasilishwa. Kwa kutumia App, unakubali masharti haya, na ikiwa hukubali, unapaswa kuepuka kutumia App.