Sera ya Faragha kwa SoteApp
Tarehe ya Kuanza: 25/03/2025
Sera hii ya Faragha inaelezea jinsi SoteApp (“sisi,” au “yetu”) inavyokusanya, kutumia, kushiriki, na kulinda taarifa zako binafsi unapoitumia Sote Mobile App (inayojulikana kama “SoteApp”). Kwa kutumia App hii, unakubali masharti ya Sera hii ya Faragha.
1. Taarifa Tunazokusanya
Tunaweza kukusanya aina zifuatazo za taarifa ikiwemo :
a. Taarifa unazotoa
• Taarifa za kaunti: Jina, email, na nambari ya simu.
• Tangazo: Maelezo ya bidhaa au huduma unayotangaza, ikiwa ni pamoja na maelezo, picha, bei, na eneo iliopo bidhaa.
• Taarifa za malipo: Ikiwa inahitajika, maelezo ya malipo (kama vile taarifa za kadi na taarifa za watoa huduma wa mitandao ya simu) kwa huduma za malipo au miamala.
• Mawasiliano: Ujumbe mfupi, kuhakiki, au maoni unayotuma kwa watumiaji wengine au kwetu.
b. Taarifa zinazokusanywa moja kwa moja
• Taarifa za kifaa unachotumia (Simu/tablet): Aina ya kifaa, taarifa ya kipekee vya kifaa, na taarifa za mtandao wa simu.
• Taarifa za matumizi: Jinsi unavyotumia SoteApp, ikiwa ni pamoja na kurasa ulizotembelea, na muda uliotumia.
• Taarifa za eneo: Eneo la karibu au sahihi (ikiwa utawezesha huduma za eneo) ili kutoa au kupata bidhaa au huduma zinazohusiana na eneo.
• Taarifa za log : Anuani ya IP, aina ya mtandao, na muda uliotumia.
c. Taarifa kutoka kwa wahusika wengine
• Tunaweza kupokea taarifa kutoka kwa huduma za wahusika wengine (kama vile mitandao ya kijamii, watoa huduma za malipo) ikiwa utaunganisha akaunti yako au kutumia huduma zao.
2. Jinsi tunavyotumia taarifa zako
Tunatumia taarifa zako kwa madhumuni yafuatayo:
• Kutoa, kudumisha, na kuboresha SoteApp.
• Kurahisisha miamala na mawasiliano kati ya watumiaji.
• Kuthibitisha utambulisho wako na kuzuia udanganyifu.
• Kukutumia updates, matangazo, na ujumbe wa msaada.
• Kuchanganua mwenendo wa matumizi na kuboresha uzoefu wa mtumiaji.
• Kufanya kazi kwa mujibu wa wajibu wa kisheria na kutekeleza sera zetu..
3. Jinsi tunavyoshare taarifa zako
Tunaweza kushare taarifa zako katika hali zifuatazo:
• Na watumiaji wengine: Tangazo lako, taarifa za profile (jina, simu,email, n.k), na meseji zinaweza kuonekana kwa watumiaji wengine.
• Na watoa huduma: Watoa huduma wa wahusika wengine ambao hutusaidia kuendesha SoteApp (kama vile watoa huduma za malipo, watoa huduma wa hosting, na watoa huduma wa mitandao ya simu).
• Kwa sababu za kisheria: Kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni, au maombi ya kisheria, au kulinda haki na usalama wetu.
• Uhamisho wa biashara: Katika tukio la kuungana, ununuzi, au kuuza mali, taarifa zako zinaweza kuhamishiwa kwa mmiliki mpya.
Hatuuzi taarifa zako binafsi kwa wahusika wengine kwa madhumuni ya masoko.
4. Usalama wa Taarifa
Tunaweka hatua za usalama kulinda taarifa zako dhidi ya watu wasioidhinishwa, mabadiliko, au uharibifu. Hata hivyo, hakuna njia ya mawasiliano kupitia mtandao ya kielektroniki inayoweza kuwa salama 100%.
5. Haki ya mtumiaji
Kulingana na eneo lako, unaweza kuwa na haki zifuatazo:
• Upatikanaji na marekebisho: Ombi la upatikanaji au marekebisho ya taarifa zako binafsi.
• Ufutaji: Ombi la kufuta akaunti yako na taarifa zako binafsi.
• Kujiondoa: Kujiondoa kutoka kwa mawasiliano ya masoko au kuzima taarifa za eneo uliopo.
• Uhamishaji wa taarifa: Ombi la nakala ya taarifa zako katika format itayohitajika.
Ili kutekeleza haki hizi, wasiliana nasi kwa soteapp1@gmail.com.
6. Uhamisho wa taarifa za zimataifa
Ikiwa uko nje ya Tanzania, taarifa zako zinaweza kuhamishwa na kushughulikiwa Tanzania- Zanzibar, ambapo sheria za ulinzi wa taarifa zinaweza kutofautiana.
7. Faragha ya watoto
App hii hairuhusu watumiaji chini ya umri wa miaka 18. Hatufanyi kukusanya taarifa binafsi kutoka kwa watoto. Ikiwa tutagundua kukusanya taarifa hizo, tutachukua hatua za kuzifuta.
8. Viungo vya wahusika wengine
App inaweza kuwa na viungo kwa tovuti au huduma za wahusika wengine. Hatuwajibiki kwa sera zao za faragha, na Sera hii ya Faragha haitumiki kwao.
9. Mabadiliko ya Sera hii ya faragha
Tunaweza kusahihisha Sera hii ya Faragha wakati wowote. Tutakujulisha kuhusu mabadiliko makubwa kwa kuchapisha sera mpya kwenye App hii au kukutumia taarifa. Matumizi yako ya App baada ya mabadiliko yanaonyesha kukubaliana na sera iliyosahihishwa.
10. Wasiliana nasi
Ikiwa una maswali au wasiwasi kuhusu Sera hii ya Faragha, tafadhali wasiliana nasi kwa:
SoteApp
Michenzania, Urban West, Zanzibar
soteapp1@gmail.com
+255 761 00 77 22